GET /api/v0.1/hansard/entries/1242973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1242973,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242973/?format=api",
"text_counter": 114,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ama ni kuruhusu nyumba zijengwe, walikuwa wapi ndiposa wananchi wanunue shamba, wajenge nyumba na waishi ndani? Kuna mzee aliye na mke na watoto na vitu vyake vya dhamana ambavyo amenunua akaweka katika hiyo nyumba. Anaamkia asubuhi moja na kupata vitu vyake vimetolewa, hana nyumba na hajui aende wapi. Kampuni ya Umeme nchini Kenya imeleta machozi mengi sana kwa Wakenya. Kubomoa nyumba bila mpangilio na idhini ya kwamba watafanya hayo siku na tarehe inayosudiwa ni kuumiza na kuhujumu haki ya Wakenya. Kwa hivyo ni makosa kabisa. Nikama Wakenya wametupa utu nje ya dirisha. Wanapofanya mambo, hawafikiri kwamba huyu ni binadamu kama mimi. Ninayetesa, kesho inawezekana ikawa ni mimi. Nitaenda wapi? Kama ingekuwa hao wamefanyiwa hayo, wenyewe wangefanya nini? Kwa hivyo, ni vizuri kuwa na utu hata kama ni kutii sheria au kuhakikisha sheria imefuatwa. Ningeomba iwe ni kampuni ya stima, watu wa mjengo au barabara, wakati wanapokabiliana na watu ambao wanadhaniwa kuvunja sheria, wawe na utu. Jambo lingine ni kuwa nchini Kenya na hasa Nairobi tunajua kwamba watu wanauziwa shamba mara mbili au tatu. Unaona mtu kwa nia nzuri ananunua shamba. Amepewa stakabadhi na anaona kwamba amenunua shamba. Baada ya miezi sita, mwingine anauziwa ile shamba na ananunua. Mwishowe, kuna mmoja atalia ama wote waumie. Wengine wanatumia stakabadhi ghushi na unapewa ukidhani ni halali. Pesa yako imepotea halafu unabaki pale ukiangaika. Hayo mambo yote yaangaliwe vizuri. Ningeomba kama ni Kamati ya Ardhi ama wanaohusika kwa Ardhilhali hii, wachukuwe hatua inayostahili. Kama ni kuchunguza kila jambo, lifanywe vizuri. Wale ambao watapoteza mali yao, walipwe rifaa. Asante sana, Bw. Spika, naunga mkono."
}