GET /api/v0.1/hansard/entries/1242987/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1242987,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1242987/?format=api",
    "text_counter": 128,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika, kama kuna wakati ambao familia huwa zinateseka ni wakati wa kufurushwa kiholela kutoka kwa makazi yao. Watu husema, uchungu wa mwana aujuaye ni mama. Hata hivyo, huwa ni uchungu kwa jamii yote kuhamishwa kutoka mahali wanaita nyumbani bila kujua pa kwenda. Wakaazi wa Chokaa ni Wakenya na wanaishi katika kijiji hicho. Hawakuchagua lakini hayo ndio makao yao. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba miaka 60 baada ya Kenya kupata Uhuru, tunafurusha Wakenya wengine kutoka sehemu wanazoita"
}