GET /api/v0.1/hansard/entries/1243136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243136,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243136/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, mimi ni Seneta wa Kaunti ya Embu aliyechaguliwa na wananchi. Kaunti ya Embu iko na sub-county nne. Nawaomba Maseneta wote 67 mhudhurie sherehe za Madaraka katika Kaunti ya Embu. Mnajua sisi kama Maseneta hatuna nguvu yeyote. Nguvu ziko katika serikali za kaunti na Serikali Kuu. Msafiri leo na kulala kule. Kesho asubuhi mfike mapema ili mpate nafasi ya kukaa. Nimeona mara nyingi Maseneta wanachukuliwa kama sio watu. Lakini nitawaambia watu wa nchi hii kuwa Senate ndio ‘upper’ House. Pili, Kaunti ya Embu inakuza miraa, majani, macademia nuts na maembe. Kule tunafanya kilimo ingawa mambo ya kilimo yako na shida kwa sababu mkulima anachukuliwa kama sio mtu."
}