GET /api/v0.1/hansard/entries/1243200/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243200,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243200/?format=api",
"text_counter": 341,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "kuchapishwa kwa paspoti nchini ambako kunaathiri mipango ya safari ya mahujaji wanaokwenda Makkah nchini Saudi Arabia kwa ibada yao ya Hajj mwaka huu. Katika taarifa hiyo, Kamati iangazie yafuatayo- (1) Iiarifu Seneti chanzo cha ucheleweshaji wa usindikaji wa Paspoti katika Idara ya Uhamiaji, ikizingatia madhara na usumbufu unaoletwa na uchelewashaji huo kwa mahujaji wanaokwenda Makkah, Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Hajj katika mwezi Juni, 2023. Ibada ya Hajj inatarajiwa baadaye mwezi ujao kuanzia 20.06.2023. (2) Ieleze ni hatua gani Serikali inachukua kuharakisha usindikaji na uchapishaji wa pasipoti hizo ikizingatiwa kwamba mahujaji watalazimika kuvunja na kughairi safari zao iwapo jambo hilo halitatatuliwa kwa haraka. (3) Ibaini ni mipango gani inafanywa na Taasisi ya Kenya Hajj Mission iliyoko chini ya uongozi wa Supreme Council of Kenya Muslims (SUPKEM), kuhakikisha kwamba mahujaji katika msimu huu wa Hajj wanapata usaidizi mwafaka ikiwepo kufuatilia na Idara ya Uhamiaji pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa kuharakisha uchapishaji wa pasipoti hizo. Asante kwa kunipa fursa hii."
}