GET /api/v0.1/hansard/entries/1243396/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243396,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243396/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Spika, swali langu la kwanza linatokana na majibu yake ya swali la 8. Kwa hivyo, ningependa unipe muda mchache niweze kuongea na Waziri. Bw. Waziri, jina ni Sen. Stewart Madzayo. Mimi ni Seneta wa Kilifi Kaunti na Kiongozi wa Wachache katika Seneti. Swali la nane linasema kwamba kulikuwa na tani 73 za mahindi, mchele na marahagwe yaliyoharibika ambayo yalichangia matatizo katika shule hiyo. Jambo la kushangaza ni kwamba hatua iliyochukuliwa na Serikali ni kutoa chakula hicho katika shule ya Wasichana ya Mukumu iliyoko katika Kaunti ya Kakamega na kukipeleka kiwanda cha Bamburi Portland Cement kule Mombasa, chini ya usimamizi wa halmashauri husika. Chakula hicho kiliharibiwa kwa sababu hakikufa kutumiwa. Jibu ulilotoa linanishangaza sana kwa sababu chakula hicho kibaya---"
}