GET /api/v0.1/hansard/entries/1243401/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243401,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243401/?format=api",
"text_counter": 78,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Bw. Spika, chakula hicho kilipelekwa katika kiwanda cha Bamburi Portland Cement kilichoko kule Mombasa ili kuharibiwa. Jambo la kushangaza ni kuwa Bamburi Portland Cement ni kampuni ya kutengeneza simiti ilhali chakula hicho kilipelekwa huko kuharibiwa. Ningependa kujua sababu ya kuchukua chakula hicho kutoka Kakamega kwenda kuharibiwa katika kiwanda cha Bamburi Portland Cement kule Mombasa ambayo ni kampuni ambayo inahusika na simiti. Pili, kwa nini ulipeleka chakula hicho kule kuharibiwa? Chakula hicho kilisafirishwa kutoka Kakamega. Kilipita sehemu nyingi sana kama vile Mlolongo ambapo kuna kampuni nyingi sana."
}