GET /api/v0.1/hansard/entries/1243403/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243403,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243403/?format=api",
"text_counter": 80,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Waziri, tafadhali nisikize. Kuna kampuni nyingi sana hapa Mlolongo zinazohusika na mambo ya saruji kama vile Simba na Rhino. Kwa nini ukawacha hizi zote, ukapeleka vyakula katika kiwanda cha Bamburi Cement kuviharibu? Si huo ni uharibifu wa pesa za Serikali kulipa pesa hizi zote kupeleka hicho chakula kiharibiwe. Hilo ni la kwanza. Bw. Waziri, ningependa ujibu swali langu sasa. Umejibu vizuri sana kuhusiana haya mambo ya Mukumu Girls’ High School. Nilivyokwambia awali, mimi natoka Kilifi Kaunti ambapo tuko na shule nyingi. Tuko na shule ambazo zinajengwa na wanavijiji wenyewe na pia za kaunti. Pia wanasiasa wanajaribu kusaidia kuinua hali ya maisha ya watoto wetu wanapoenda shule kusoma. Kuna shule moja inayoitwa Amason Jeffa Kingi (AJK), Adu Ward, Uwakilishi Bungeni wa Magharini, Kilifi Kaunti, ambapo mimi ninawakilisha. Ninaomba kujua ni lini utafanyia shule hii mipango? Shule hii imepata taabu sana kwa sababu ya uhaba wa walimu? Wale wakaazi wa hapo wamekuwa wakilipa walimu. Wakati mwingine wanaposhindwa, walimu wanakosa kufundisha kwa sababu hawajapata malipo yao ya mwisho wa mwezi. Ni lini Serikali itaweza kupeleka walimu wa Serikali katika shule hiyo? Ni lini Serikali itachukau hatua ya kumiliki hii shule na kuajiri walimu ili wakaazi wa eno hilo wapate afueni?"
}