GET /api/v0.1/hansard/entries/1243413/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243413,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243413/?format=api",
    "text_counter": 90,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chute",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13583,
        "legal_name": "Chute Mohamed Said",
        "slug": "chute-mohamed-said"
    },
    "content": "hivyo nikaelezwa kuwa hawana facility ya kutosha ya kuweka chakula hicho. Chakula hakiharibiki kwa sababu ya vile kinavyo safirishwa pekee. Hata vile kinahifadhiwa katika magala kinaweza kuharibika. Nimemsikia Bw. Waziri akizungumza juu ya mambo ya shule moja pekee yake. Ni mikakati gani Wizara yake imeweka kuhakikisha shule zote nchini zina mipangilio mizuri ili shida kama ya shule hii izitokee tena? Ninajua Bw. Waziri yuko na maofisa wa kutosha wakumujulisha mambo yote kushusu elimu yanayoendelea kila mahali nchini. Umetuambia hatua ambayo umechukua katika shule hiyo, lakini hujatuambia hatua ambazo utachukua kuhakikisha usalama wa wanafunzi katika shule zingine nchini. Leo, hatujui ni wanafunzi wangapi nchini watakufa kutokana na shida kama iliyokuwa katika ya upili ya Mukumu. Shida hiyo sio shule pekee, lakini ni shisa pia katika shule nyingi hapa nchini. Ni hatua gani umechukua ili tusipoteze watoto na walimu tena katika shule ya Mukumu High School? Asante sana."
}