GET /api/v0.1/hansard/entries/1243560/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243560,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243560/?format=api",
"text_counter": 237,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii nichangie Hoja iliyoletwa na rafiki yangu, Sen. Kibwana. Hii ni Hoja ya maana sana. Ni kwa sababu kwanza tulipokula kiapo tukiwa tumeinua Biblia kama viongozi katika nchi hii, kila mmoja wetu alipata haki ya kulindwa. Kwa hakika, wanaotulinda ni askari. Tunazungumzia maisha ya askari walio na umuhimu mkubwa sana nchini. Afia ya akili ya askari inachangiwa sana na kazi wanayofanya. Kazi waifanyayo iko na matatizo chungu nzima. Wengi waliyonitangulia wamezungumza na kusema kwamba askari hao katika kitengo chochote kile, wanaishi katika mazingira duni. Nyumba zao hazipendezi kamwe. Wanaishi kama wanafunzi shuleni. Hawana faragha. Hawaishi maisha yao kama binadamu mwingine yeyote. Wanaishi kwa vyumba ambavyo kila mtu anaweza kuchungulia, kuingia na kuketi. Hawajisikii kama wana faragha ama maisha yao ya kibinafsi. Mambo haya yote huchangia kwa sababu tumeamua kuweka askari wetu katika mazingira duni. Jambo lingine ni kuhusiana na kazi wanayofanya. Tunapolala, huwa tumetosheka na hali ya usalama manyumbani kwetu. Hao ndio hutulinda na kuhakikisha tuko salama. Kuanzia kwa Rais, Mawaziri, Wabunge na wengine wote. Tunapofurahia na kulala vyema bila wasiwasi wowote, wao wako msituni, mashimoni, kwa mahandaki na kwa miti. Wengine wanalala huku wanalinda malango yetu. Wakati Kiranja wa Walio Wengi, Sen. (Dr.) Khalwale, analala vizuri, askari ako pale langoni kuhakikisha magari, mali, wanyama, watoto na wake wake wengi wako sawa."
}