GET /api/v0.1/hansard/entries/1243562/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243562,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243562/?format=api",
    "text_counter": 239,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ni kwa nini tusishughulikie masilahi ya askari wetu? Jambo lingine, ninashukuru kwa hii nafasi maana imenipa fursa kuzungumzia jambo ambalo ni la muhimu sana. Jambo lenyewe ni mshahara. Askari anapata mshahara wa shilingi 15,000. Akichukua mkopo, anakatwa yote. Mwisho wa mwezi, anapokea shilingi 1,500 na ako na watoto shuleni, majukumu ya boma, bibi wa kupeleka salon, watoto wa kupeleka shule na anahitaji kukula bacon kama mimi. Tunatarajia aje aishi maisha mazuri ya kufurahia akiwa amewekwa kwa mazingira ya aina hii kwa sababu tumeamua tusiwalipe vizuri? Kwa nini Serikali ya Kenya isiamue askari wapate mshahara mkubwa?"
}