GET /api/v0.1/hansard/entries/1243564/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243564,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243564/?format=api",
    "text_counter": 241,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, jambo lingine ni wananchi tunachangia askari kuwa na matatizo ya kiakili. Hi ni kwa sababu atuwakubali. Ni kama wao sio wananchi. Tunawaona ni kama maadui. Hawajiskii kama wao ni Wakenya wenzetu. Hawakubaliki kwa jamii. Ukiona askari, unakata kona. Mara nyingi, nikitembea barabarani, ninaona hustlers wanaouza vitu vyao, wakinong’onozewa huyo ni askari, wanakata kona na kukimbia mbio kana kwamba ameona mnyama. Kwa nini tusiishi na askari kama marafiki? Ni ndugu, baba na watu wetu kwa jamii. Kwa hivyo, tuwe na mazoea ya kuishi na askari kama binadamu wenzetu. Tuwakubali, tuwe marafiki wao na tuwe karibu nao bila kuwalaumu kwa jambo lolote. Ukiona askari, unafikiri ataitisha hongo, atakukamata au ni adui. Kwa nini tusikubali askari wakuwe kama sisi wanasiasa ambao kila mtu anataka kutangamana nasi, kutukaribia na kutuomba hiki na kile. Askari akikubalika kwa jamii, hatakuwa na tatizo la kiakili. Lakini, matatizo ya kiakili yanachangiwa na kutokubalika na kujiona kwamba wao sio binadamu au kazi walioichagua si nzuri ama haihitajiki nchini Kenya? Bw. Spika wa Muda, ningeomba Waziri wa Mambo ya Usalama wa Ndani na wote wanaohusika waangalie maslahi ya askari nchini Kenya. Kwa hakika, kama vile dada yetu amependekeza kwa Hoja hii, ingewezekana hata kama ni hospitali ijengwe. Askari yeyote akionekana ako na tatizo, akimbizwe na ahudumiwe vilivyo kuliko kuachiliwa na kuanza kuchekelewa, kulaumiwa na kuonekana kama hafai au nimakosa yake kuwa vile alivyo. Tunajua kwamba askari pia wako na cheo na wengine wanafanya kazi kwa changamoto nyingi sana. Wale askari wa kiwango cha chini, huwa wanakanyagiwa chini. Wengine wamefanya kazi miaka nenda, miaka rudi, na hawapandishwi cheo. Hii ni kwa sababu kama hawajui ‘nani ni nani,’ basi wataendelea kupitwa. Hawapandishwi cheo na hakuna mtu anatambua kazi wanayofanya. Wengi wao watapatwa na matatizo ya kiakili. Maana anashindwa atafanya kazi kwa kiwango moja tu bila kupandishwa cheo. Kama alianza kama private member, anaendelea tu mpaka mwisho. Baba yangu, ndugu zangu, brothers-in-law na jirani yangu wote ni askari lakini nikiwatazama, ninawahurumia. Ni kazi lakini hawajivunii kuwa kwamba wanafanya kazi. Ni muhimu tushughulikie jambo hili kwa ufasaha kuhakikisha kwamba watoto wetu, ndugu zetu, mabwana zetu na majirani zetu ambao ni askari wamewekwa kwa kiwango ambachoo hakitawaruhurusu kupatwa na matatizo ya kiakili. Kwa mambo ya mapenzi, hakika tumeshuhudia nchini Kenya shida nyingi sana kuhusu mapenzi kwa askari. Unaskia askari ameua mwenzake kwa kumpiga risasi. Ni kwa sababu kama amepata rafiki kama binadamu yeyote yule, anataka kumweka kiwango kile cha kufurahisha pia naye askie kwamba anasonga na maisha vizuri. Lakini, matatizo ya kimfuko na kuonekana ni mtu wa kiwango cha chini inamfanya afanye mambo yasiyostahili. Wengine wananyang’anywa wapenzi wao na wakubwa wao na hawawezi fanya chochote. Kwa mazingira na wakati kama huo, askari atakuwa na matatizo ya kiakili."
}