GET /api/v0.1/hansard/entries/1243566/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243566,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243566/?format=api",
    "text_counter": 243,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ni muhimu Hoja hii ishughulikiwe. Mazungumzo ya siku ya leo yasiishie hapa. Hatua ichukuliwe tuonekane kwamba tunajali maaskari na usalama wetu. Maana, tukiwaweka kwa mazingira duni na kwa mambo ambayo hayafurahishi maishani, wanahangaika saa zote. Watalinda usalama wetu aje? Ndiposa wengine wanaanguka kwa majaribu ya kuchukua kitu kidogo. Si mapenzi yao. Huenda ikawa hata imani na dini yake haimruhusu afanye hivyo. Lakini, kwa sababu ni binadamu na ako na mahitaji, anaagukia kufanya mambo yasiyostahili na sio vizuri. Bw. Spika wa Muda, ninaunga mkono Hoja hii. Hatua madhubuti ichukuliwe kuhakikisha kwamba askari wetu hawana matatizo ya kiakili. Wale kwa bahati mbaya wanapata matatizo ya kiakili, wanashughulikiwa ipasavyo."
}