GET /api/v0.1/hansard/entries/1243641/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243641,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243641/?format=api",
"text_counter": 60,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Mashirika haya yanapaswa yapigwe msasa na yaangaliwe kwa undani. Mashirika mengine yamekuwa yakijihusisha uporaji, kuwaibia na kuwalaghai wananchi wa Kenya. Kwa hivyo, Serikali inapaswa ishughulikie jambo hili kwa sababu wananchi wengi wamekuwa wakigandamizwa na mashirika haya. Katika nchi yetu ya Kenya, watu wengi wanatafuta ajira. Mashirika haya yanachukua jukumu hilo kwa sababu wanajua watu wengi wanatafuta ajira. Mashirika haya wanawaitisha hongo na pesa watu wanaotaka kuajiriwa. Jambo la kuvunja moyo zaidi ni kwamba mashirika haya hayawatafutii Wakenya kazi baada ya wao kujitolea mhanga kuwapa pesa zao. Wanabaki kuwalaghai watu wetu. Ni vizuri mashirika haya ambayo yanajihusisha na hayo mambo, yakuwe yameangaziwa ndiposa Wakenya waweze kuwa na imani na hayo mashirika. Bw. Spika, tumeona wananchi wa Kenya wakipata tabu, maafa, kuchapwa na hata wengine wananajisiwa kwa sababu wamechukuliwa na mashirika haya na kupelekwa katika nchi za kigeni. Utapata kuwa wanabaki katika mikono ya wakora hawa. Kwa hivyo, Serikali iangazie jambo hili. Ninataka kumpongeza Sen. Cherarkey kwa kuwa mstari wa mbele kushughulikia haya mambo. Ninajua yeye ni mwanaharakati wa chama cha United Democratic Alliance"
}