GET /api/v0.1/hansard/entries/1243654/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243654,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243654/?format=api",
"text_counter": 73,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Kwanza, nampatia kongole ndugu yangu kwa kuleta hii Taarifa wakati huu ambao unafaa. Tunaelewa kwamba watoto wetu wengi wanaenda kutafuta mapato katika nchi za ughaibuni. Mara nyingi wakiondoka hapa, huwa tunajua anwani zao na namba za simu zao za mkono. Hata hivyo, mara tu wanapofika kule, huwa ni shida sana kuwafikia. Tumekuwa na vifo katika utendakazi wao na kupoteza maisha. Senator wa Kaunti ya Nandi; mchapa kazi, amefanya jambo jema sana kwa kuandika Taarifa yake ya kwamba ni lazima zile kampuni ambazo ziko hapa na zinachukua watoto wetu na kuwapeleka kule kwenda kufanya kazi ziajibike. Inafaa wanajue kule watu wetu wanaenda. Wakati wowote shida ikitokea, tunaweza kuwauliza swali hili. “Watoto wetu mliwachukuwa mkawapeleka pahali fulani, sasa wamesema ya kwamba kuna shida, wanatakikana warudi.” Bw. Spika, kuna upungufu. Hatuna njia ya kujua watoto wetu wanaotoka hapa na kwenda nchi za uarabuni kufanya kazi, wakifika kule watafanya kazi wapi. Hata hivi, juzi nikiwa nyumbani wiki hii, kuna mtoto aliondoka kwenda kufanya kazi huko. Tangu alipoondoka, ni karibu miezi minane sasa na hajapiga simu nyumbani na ni mtoto wa kike. Hatujui kama yuko sawa kule aliko enda ama hayuko sawa."
}