GET /api/v0.1/hansard/entries/1243695/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243695,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243695/?format=api",
"text_counter": 114,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Kwanza, ni hoja nzuri sana kwa sababu sijawahifika Kaunti ya Turkana. Kwa hivyo, nitapata nafasi ya kuweza kuonana na ndugu zetu Waturkana. Itakuwa jambo nzuri zaidi kuwa hili Bunge letu la Seneti litakuwa na kikao huko Kaunti ya Turkana. Tukiangalia katika miaka karibu 50, nchi inayoitwa Dubai ilikuwa ni jangwa; hakukuwa na rasilimali yoyote kule. Ilikuwa haijawahi kuonekana. Miaka 50 iliyopita, ukifika kule hivi sasa, siyo jangwa tena."
}