GET /api/v0.1/hansard/entries/1243697/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243697,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243697/?format=api",
    "text_counter": 116,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Vilevile, katika nchi yetu hii ya Kenya, Kaunti ya Turkana, ni mahali ambapo kampuni ya Tullow Oil Company imeweza kuona ya kwamba kunayo mafuta ya maana sana katika ulimwengu. Wengine tutakuwa hatuko huko. Ninaona katika hii Seneti, watakaobaki ni akina--- ndugu yangu mdogo. Pengine wakati huo watakuwa wamefika miaka ya kuhesabu. Kenya itabadilika wakati sisi tutaanza kuchimba hayo mafuta, kuyauza na kupata pesa. Bw. Spika, pia ni jambo nzuri kuona ya kwamba sisi tutaongeza uhusiano zaidi. Nina hakika kuna watu wengine ambao wameishi Kaunti ya Turkana mpaka hivi sasa hawajawahi kukutana na Maseneta wengine kutoka kaunti zingine. Itakuwa nafasi nzuri kuwa na uhusiano mwema na watu wa kaunit hiyo. Tutaweza kukaa nao, kuongea na wao waweze kuona vile taratibu za Seneti hufanyika na kujifundisha mengi kutoka kwetu. Hata wakimchagua Seneta wao, ndugu yangu, Sen. Lomenen. Hayuko leo lakini akiwa, yeye kama Seneta wa Kaunti ya Turkana, tunajua ni shupavu na watu wake walimchagua aje hapa ili aweze kutetea haki zao. Watu wa Kaunti ya Turkana wataweza kujua maana ya kuwa ndani ya Seneti, Seneta anavyofanya kazi na uwezo wake uko namna gani wakati tukiwa kule. Tutaweza kupata nafasi nzuri pia ya kuweza kuwaeleza hususan kazi za Seneti ni nini ili waweze kuelewa. Bw. Spika, nashukuru kwa kunipa muda huu."
}