GET /api/v0.1/hansard/entries/1243736/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243736,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243736/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Bw. Spika, asante kwa nafasi hii. Kwanza ni kushukuru waliohusika kuchagua Turkana kama eneo lililoteuliwa kwa Seneti kufika na kufanya mkutano huko. Kihistoria, eneo la Turkana limekuwa eneo ambalo limetelekezwa. Ni eneo ambalo Wakenya walikuwa wanasikia tu kuhusiana na maisha ama vita dhidi ya wanaoishi katika maeneo hayo. Kwa sasa, kutokana na uamuzi wa Seneti, tutakwenda kule mashinani kukutana na wananchi. Vile wenzangu wamesema, itakuwa wakati mzuri kupiga msasa hatua za ugatuzi kwa miaka kumi fedha ambazo tumekuwa tukipitisha kwenye Bunge la Seneti ziwe zinakwenda mashinani. Pesa hizi zitaweza kuonekana. Kama ni maji yalichimbwa na kuna vidimbwi vya maji. Iwapo ni barabara, je ilijengwa? Pesa zilitengwa kwa ukulima na mifugo, tutajionea kwa macho iwapo hizo pesa zimeafiki malengo ya ugatuzi kule Turkana ama kuna wachache ambao wamekuwa wakizigatua kibinafsi na kufanya miradi ya maendeleo kule Turkana. Vilevile yale ambayo yamekuwa yakiibuka kama vile vita dhidi ya jamii husika kule Turkana na majirani zake, tutaweza kufika na kujionea kwa macho. Tutaweza kuwasikiza wenyeji ili tunaporudi katika mipangilio na ratiba ya Seneti, tusimame kidete na ugatuzi na kuhakikisha kwamba watu wa Turkana na majirani wao wanaishi kwa umoja na upendo. Hivyo basi, Kenya itasonga mbele. Jambo lingine ambalo lazima tutaweza kuangazia ni mipaka yetu na nchi yetu jirani ambayo Turkana inapakana nao. Kwa muda mrefu jinsi tumeona kwa vyombo vya habari, Mhe. Rais wa nchi jirani ametoa amri kwamba wale waliohusika kwa vifo vya Waganda kule Uganda, wasalimishwe katika vyenzo vya sheria nchini humo ama Waturkana wafurushwe wote warudi Kenya. Seneti itakuwa na nafasi ya kuwa kiunganishi ama kipatanishi kati ya idara na nchi mbalimbali kuhakikisha kwamba Wakenya ambao wanaishi kule Uganda hawaumii kwa sababu ya makosa ya watu wachache. Sen. (Dkt) Oburu amesema, sisi kama Serikali ya Kenya Kwanza, tulikuwa na mkataba na wananchi. Tulifanya vikao katika kaunti zote. Tulipokuwa kule Turkana, tuliahidi Wakenya kwamba unyunyiziaji wa mashamba utaweza kuimarishwa ili wawe na mbinu mbadala ya kupata chakula bila kutegemea mahindi peke yake. Kamati yetu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ingependa kujua Serikali imefanya yapi kuhusiana na mpangilio wetu wa kuimarisha ukulima kule Turkana na ufugaji wa mifugo ili kuimarisha kipato cha mifugo ili watu wa Turkana watambuliwe kwamba wako Kenya. Napendekeza kwamba katika maeneo mengine tutakayozuru, kwa mfano, juzi tulikuwa na Waziri wa Nishati na Mafuta hapa. Ndugu yetu kutoka Turkana aliuliza maswali ambayo yalikuwa yamemkera na Waziri alipoondoka, bado ndugu yetu Seneta hakuwa ameridhika."
}