GET /api/v0.1/hansard/entries/1243738/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243738,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243738/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Tutakapozuru maeneo mengine, tutakuwa tunawaalika wale Mawaziri ambao Wizara zao zinaafiki malengo hasa ya kaunti tunayozuru ili wenyeji wa kaunti hizo wasikize Mawaziri hao kutoka mashinani. Iwapo hawaleti majibu yanayostahili, wananchi vile vile wasitusulubishe sisi Maseneta na viongozi lakini waweze kujua ni nani ambaye hafanyi kazi ambayo alitumwa ama aliyopewa na Serikali. Ninaunga mkono hatua zetu za kwenda kule. Na nikimalizia, kumekuwa na donda sugu la walimu kutoka maeneo mbalimbali kufunza maeneo tofauti. Tutakapokuwa kule, tutataka kujua walimu ambao walihama kwenda maeneo mengine na wale walioko wanaafiki idadi ya wanafunzi na changamoto au kuna dosari ya elimu kule Turkana. Kwa sababu tukiweka kwenye ramani na mchakato wa manufaa ya elimu, naamini kwamba Turkana inajizatiti lakini bado haijafika kiwango ambacho kinastahili. Naunga mkono hatua hii na kuomba Wakenya kule Turkana wajitokeze, watazame kwenye vyombo vya habari wale ambao watapata nafasi ya mtagusano na sisi tuweze kupata mwelekeo unaostahili kutokana na nafasi zetu. Mwisho, wengi kama vile Kiongozi wa Walio Wachache Seneti, Sen. Madzayo, alivyosema, kuna vigogo kihistoria na kisiasa lakini bado hawajatembea Kenya ili waelewe Wakenya wanaumia namna gani. Hii ni nafasi Wakenya wajue viongozi hawa ambao wanavuma wakiwa baharini, huku mashinani wanajulikana ama hawajulikani ama wana hoja ama hawana hoja, ama wanaelewa Kenya ama hawaielewi. Wengi tumekita mizizi tu kupiga siasa za hekaya ya Abunuwasi lakini maisha ya Mkenya yanayomkera kule mashinani bado hawajui. Nashukuru Seneti na Spika haswa kwa kuwapeleka watu mashinani ili wajue kwamba ijapo tuko Nairobi, kila kitu kinatoka kijijini. Asante, Bw. Spika."
}