GET /api/v0.1/hansard/entries/1243748/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243748,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243748/?format=api",
    "text_counter": 167,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Kwanza, naunga mkono Hoja hii. Ibara ya 96 ya Katiba ya Kenya inasema kwamba kazi kuu ya Seneti ni kulinda na kutetea gatuzi zetu. Itakuwa jambo la kuvunja moyo ikiwa tutasema ya kwamba tunatetea gatuzi zetu na hatuzifahamu na hata hatujui pahali ziko. Kwa hivyo, tutakuwa tukifanya jambo la muhimu kuitembelea Turkana. Nilisikia Kiongozi wa Wachache akisema hajatembea sehemu hiyo. Si yeye pekee bali wako wengi. Itakuwa ni jambo nzuri sisi kutembelea gatuzi zetu ili tuweze kujua masaibu na changamoto wale wanaoishi pale wanapitia ama vile vile mambo ya manufaa wanayoyatenda ambayo sisi tunaweza tukaiga katika kaunti zetu. Bw. Spika, ningeomba Kamati zetu ziweze kuwa na vikao pale. Kwa mfano, jambo la usalama ndilo swala ambalo limekuwa likisumbua ndugu zetu wa kutoka Turkana. Kwa hivyo, Kamati yetu ya usalama ikiwa pale itaweza kulivalia njuga suala hili na pengine wakiwa pale, wateweza kuona jinsi watatua jambo lilo. Bw. Spika, katika Kamati ya Elimu, tumeeambiwa kwamba Gavana Nanok alijenga shule nyingi za chekechea. Itakuwa ni fursa nzuri kwa Mwenyekiti wangu ambaye ni Sen. Joe Nyutu kutoka Murang’a, kutembea na kuona kama zile hela ambazo walipewa zilitumika kwa njia inayofaa na tuweze pia kuiga mambo yaliyofanyika pale na tuyapeleke katika gatuzi zetu. Hilo ndilo jambo ambalo litasaidia sana. Ikiwa tutakuwa tunatembea tu bila kujifunza jambo lolote ambalo tunaweza kupeleka katika gatuzi zetu, basi haitakuwa na haja. Bw. Spika, jambo lingine la muhimu ni kwamba, wengi wa wale ambao wako katika gatuzi zetu hawafahamu kazi ya Seneti. Unapata unapotembea mashinani unaambiwa kwamba tumeona gavana ametengeneza barabara, Mbunge ametengeneza shule ya msingi lakini hatujaona Seneta akifanya jambo lolote. Kwa hivyo, tukitembea katika gatuzi zetu, hao wananchi wataweza kufahamu kwa sababu tutashirikiana nao, wataona tukijadili na wataweza kufahamu kwa kindani kazi ya Seneta. Bw. Spika, nakumbuka tulitembelea gatuzi ya Uasin Gishu. Tuliweza kuangazia mambo ya kilimo. Kamati yetu ya Kilimo iliangazia shida za mambo ya mahindi zilizokuwepo wakati ule. Wakenya waliweza kujieleza kinagaubaga na tukaweza kutatua shida walizokuwa nazo wakati ule. Bw. Spika, siyo kilimo peke yake. Kamati ya Afya iliweza kutembelea Moi Teaching and Referral Hospital na tukaweza kutatua shida zilizokuwepo hapo kwa sababu tulikuwa na wakati mwingi; sio kutembea tu na kurudi Nairobi. Tulikuwa na wiki nzima katika mji ule. Bw. Spika, nina uhakika tukitembea Turkana, Kamati zote zitakuwa katika Kaunti ya Turkana. Kwa hivyo, nina uhakika tutaweza kutatua changamoto, masaibu na shida zote walizonazo kwa sababu tutakuwa katika gatuzi hilo. Bw. Spika, ijapokuwa ninasema tutaenda katika Kaunti ya Turkana, taarifa niliyonayo ambayo siwezi nikaisema kwa undani ni kwamba Laikipia ndiyo iliyokuwa imepewa kipaombele. Sijui ni lipi lilifanyika ikasemekana kwamba tuende Turkana, lakini nakubali na naunga mkono."
}