GET /api/v0.1/hansard/entries/1243759/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243759,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243759/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "unakwenda kwa gari kama walalahoi au “mahustlers” wengi. Baaadaye, siku ya pili uendelee na safari mpaka Lodwar. Bw. Spika, hii itatoa fursa kubwa kwa Bunge la Seneti kusoma maeneo ya Turkana na maeneo jirani. Vile vile, itatoa fursa kwa watu wa Turkana kusoma Bunge lao linafanya kazi namna gani. Itakuwa ni fursa ya Bunge la Kaunti ya Turkana kupata fursa ya kuona vikao vya Seneti na vile kamati tofauti tofauti za Seneti zinavyofanya kazi. Kamati hizi ama mabunge haya ya kaunti, mara nyingi huwa yamelema kikazi kwa sababu ya kutopata nafasi ya kusoma kutokana na vile kazi zinavyotendwa katika mabunge mengine. Bw. Spika, hii itatoa fursa kubwa kwa bunge la Kaunti la Turkana kusoma vile kamati zetu zinafanya nini na kuhakisha kwamba zile taratibu za mabunge yote zinafuatwa kama inavyotakikana. Ningependa kuomba wakati wa ziara hii, Kamati ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu izuru mahakama na gereza ya Turkana ili kuona vipi wafungwa kule wanaangaliwa kulingana na sheria. Mara nyingi zile mahakama na gereza ambazo ziko nje ya miji mikubwa, kuna dhuluma nyingi sana za haki za binadamu ambazo hazipatikani kuelezwa ama kutambuliwa ilihali Kenya ina Katiba moja na sheria moja ambayo inawalinda wafungwa popote pale walipo. Ningeomba kwamba kuwe na ziara katika gereza hilo ambalo liko Turkana na pia mahakama ya Turkana ili tuone kwamba wananchi wanahudumiwa kisheria kama inavyopaswa katika nchi yetu ya Kenya. Bw. Spika, mwisho tutapata fursa ya kujua mbinu za kutumia ili kusaidia Kaunti ya Turkana kuweza kuongeza own source revenue sababu pesa ambazo zinatoka katika Serikali ya Kitaifa hazitoshi. Ijapokuwa zinaongezeka, ukizingatia huduma ambazo zinatakikana kutolewa na kaunti, pesa ambazo zinapelekwa huko hazitoshi ikilinganishwa na wakati ugatuzi ulipoanza. Tutapata fursa ya kuona jinsi huduma za afya zimeweza kuboreshwa nchini Kenya kulingana ugutuzi. Bw. Spika, vikao hivyo vitakuwa muhimu sana, sio tu kwa Seneti peke yake, bali kwa watu wa Turkana na nchi nzima kwa jumla. Tutapata fursa ya kutembelea na kuona hali ya Wakenya wenzetu katika Kaunit ya Turkana. Asante sana."
}