GET /api/v0.1/hansard/entries/1243934/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243934,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243934/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bwana Spika, ningependa kuchukua nafasi hii kutoa salamu za rambirambi zangu pamoja na familia yangu na watu wa Kaunti ya Tana River, kwa jamaa na marafiki wa familia hii ya Seneti. Sisi tukiwa hapa ni wachache. Lakini, Mwenyezi Mungu, kwa mipango yake ametuondolea mmoja wetu katika familia hii. Wakati mwingine hatuna majibu kwa maswali maanake kuna wale wengine ambo ni wengi zaidi. Hatusemi angechagua kule lakini ni wengi zaidi kuliko huku. Lakini, Mwenyezi Mungu aliona achukue mmoja wetu. Tunasema pole kwa sisi sote haswa wale waliokuwa wakifanya kazi karibu na yeye. Pili, ninatoa pia rambirambi zangu kwa familia ya Makamu wetu wa Rais wa zamani, Mzee Moody Awori, ambaye tulifanya kazi naye. Tunasema pole sana. Sisi ambao ni wazazi, hua hatuombi na hatutarajii ya kwamba watoto wetu watatembea kwenda mbele ya haki kabla yetu. Kwa hivo tunasema pole sana kwa Mzee, familia na sisi sote. Mungu atupe nguvu kwa wakati huu mgumu na atupatie neema tuweze kupitia wakati huu."
}