GET /api/v0.1/hansard/entries/1243958/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243958,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243958/?format=api",
    "text_counter": 61,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Ninachukua fursa hii kuleta risala za rambirambi za familia yangu pamoja na watu wa Kaunti ya Laikipia. Bw. Spika, ninataka kuungana nawe kusema pole kwa familia kwa sababu ninamjua vizuri sana Bi. Marya. Muda uliopita, nilipokuwa Spika wa Muda, tulifanya naye kazi vizuri kwa karibu na nilimjua kama mtu aliye makinika katika kazi yake. Sitasahau ya kwamba, Bi. Marya aliongea kwa lugha ya Kiingereza akimakinika kabisa. Ninakumbuka vizuri sana kila wakati nilipokuwa pale akija, alikuwa akinileleza kwa sababu ilikuwa mara yangu ya kwanza kuketi katika kiti hicho, nilimtegemea yeye sana. Namkumbuka nikiwa na uchungu kwa kumpoteza. Ni jambo la kuvunja moyo wakati sisi tunaoongea hapa kila wakati tukiomboleza ndugu zetu. Nakumbuka nilisimama hapa mara ya kwanza nikimwomboleza Mheshimiwa Ben Aluoch, tena nikasimama nikimwombleza Mheshimiwa Sen. Kabaka. Tena nikasimama hapa nikimwomboleza Bw. Wellington Namenge. Na hivi sasa kwa uchungu tena ninasimama kumwomboleza Bi. Marya. Ijapokuwa Bibilia inasema kuwa Mungu hajibu maswali ila hujibu maombi, sisi kama binadamu tuna uchungu kwa kumpoteza mmoja wetu ambaye tulifanya naye kazi. Kwa familia, ninawaambia pole, hata ijapokuwa hiyo ndiyo njia hata sisi ambao tunangoja tutaipitia, tujiulize tu maswali, wakati wetu utakapofika, mimi Sen. Kinyua, nitakuwa ninamjua Mungu kwa njia gani? Kwa sababu hiyo ndiyo njia na ninangojea---"
}