GET /api/v0.1/hansard/entries/1243967/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243967,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243967/?format=api",
    "text_counter": 70,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii ili niweze kujiunga na wenzangu kutoa rambirambi zetu kwako, kwa Katibu wa Bunge na familia ya mwendazake, Bi. Marya Adjibodou. Bw. Spika, kwa hakika ni pigo kubwa, sio kwa familia yake peke bali pia kwa Bunge hili la Seneti. Bi. Marya alikuwa mfanyikazi ambaye alikuwa anafanya kazi yake kwa uangalifu zaidi na kwa haraka, iwapo atahitajika kufanya hivyo kwa haraka. Bw. Spika, nilimjua Bi. Marya kutoka mwaka wa 1980 tulipokuwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Alikuwa akisomea Bachelor of Arts na mimi nilikuwa nikisomea uanasheria. Nilimpata hapa nilipokuja kwa muhula wangu wa kwanza na baada ya kuzungumza na yeye, tukajuana kwamba ni kweli tulikuwa mwaka mmoja katika Chuo Kikuu. Mwaka uliopita, tulisafiri nayee kwenda France kwa maswala ya ACP-EU. Kwa hakika, mara nyingi alikuwa mtu mwenye usaidizi mkubwa katika safari hizo, sio tu kwa mambo ya kawaida ya usaidizi wa protocol, lakini pia kwa yale maswala ambayo yanayozungumziwa katika mikutano hiyo. Alikuwa na umahiri na kwa hivyo, alikuwa wa msaada mkubwa kwetu sisi ambao tulikuwa tunashiriki katika mikutano ile. Bw. Spika, hiyo ndiyo njia yetu sote. Sisi Waislamu husema, “ inna lillahi wa inna"
}