GET /api/v0.1/hansard/entries/1243970/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243970,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243970/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante sana kwa nafasi hii. Kwa niaba yangu, familia yangu na watu wa Bungoma, ninatoa rambirambi kwa familia ya mwendazake. Nilimjua kama mama mcheshi, mkarimu na mpole, ambaye hakuwa na majivuno ama kujigamba. Alikuwa mchapakazi ambaye alijitolea kwa hali na mali kuhakikisha kwamba mchango wetu katika Seneti inahakikiwa na kunakiliwa kwenye kumbukumbu za Jumba la Seneti na kuhakikisha kwamba Kenya inapata haki kwa kipato kidogo, kile ambacho Wakenya wanatozwa. Bw. Spika, vile vile, ningependa kutoa rambirambi kwa familia ya mwendazake, kwa sababu wahenga walisema kwamba tunda hili la binti huyu lilianguka kwenye shina la mti na ukiashiria vyema, unaona taswira ya Mhe. Moody Awori. Ni kielelezo kwa wengi wenye tajriba, pesa, uzoefu wa kisiasa na uzoefu wa kushika hela. Kwamba, japo hadhi ya wazazi wako katika nchi yetu, ni lazima tuwe wapole, wakarimu na wachapakazi, kama vile marehemu alivyojieleza na kufanya kazi katika Seneti."
}