GET /api/v0.1/hansard/entries/1243980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1243980,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243980/?format=api",
    "text_counter": 83,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa nafasi hii, kutoa rambirambi zangu kwa familia ya Marya. Tulijuana na Marya nikiwa Bunge la Kitaifa kabla nije hapa Seneti. Tulifanya na yeye kazi vizuri sana. Nimewahi kusafiri na yeye. Hata nilipokuwa nikipata mjukuu wangu wa kwanza, Marya aliwahi kumnunulia zawadi nilipokuwa nikimfanyia shopping . Bw. Spika, Marya alikuwa karani mtaalamu ambaye alikuwa akifanya kazi yake kwa uadilifu sana. Ni masikitiko kwamba hayuko na sisi leo. Alikuwa karani ambaye ni msaidizi mkubwa kwa kila mfanyikazi na kila Seneta. Leo hii hayuko na sisi lakini tunasema sisi waislamu, “kulu nafs dhayigat al mawt.” Kila nafsi itaonja mauti. Binadamu wote watakufa, kila mtu na siku yake. Jambo la muhimu ni sisi sote kuhakikisha na kudhibitisha kwamba tunawacha mambo mazuri nyuma baada ya kuondoka, kama vile tunamwongelelea mwenzetu Marya kwa uzuri. Sisi sote ni mashahidi wa Marya kwa sababu aliishi na watu vizuri. Sisi ndio tutakuwa mashahidi wake kule aliko, mbele ya Mwenyezi, kwa kumwongelelea vizuri kwa sababu aliishi vizuri. Natoa rambirambi zangu kwa familia, bwana yake, watoto, Katibu wa Seneti na pia kwako Bw. Spika. Asante sana."
}