GET /api/v0.1/hansard/entries/1243993/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1243993,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1243993/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13592,
"legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
"slug": "onyonka-richard-momoima"
},
"content": "Bw. Spika, kwa niaba yangu kama Seneta wa Kaunti ya Kisii, kama kijana wa aliyekuwa Mbunge wa Kitutu Chache zamani, Dr. Zachary Onyonka, ambaye alifanya kazi na mzee Moody Awori, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa familia ya mzee Awori, kwako wewe binafsi kama Spika wetu na wafanyikazi wote wa Seneti. Bw. Spika, mama Marya ni mtu tulikuwa tunamheshimu. Unavyojua, nimekaa hapa kwa muda na nimekuwa nikimwona wakati Seneti ilipofunguliwa. Amefanya kazi tangu nikiwa Mbunge katika Bunge la Kitaifa . Pole kwa familia, marafiki na wale wote ambao wamehusika kwa kuchangia na kuhakikisha kuwa amefanya kazi nzuri kwa hili Bunge la Seneti. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Shukrani."
}