GET /api/v0.1/hansard/entries/1244851/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1244851,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1244851/?format=api",
    "text_counter": 125,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante Bw. Spika. Kwanza, ninamshukuru ndugu yetu, Sen. Cherarkey, Seneta wa Kaunti ya Nandi. Kama kuna askari ama first-hand solders wa devolution ni MCAs wetu. Bila hao, hakuna devolution kwa sababu hao ndio wanahusika na watu directly. Sisi tukienda kule, inakuwa ni baada ya kuunda policy hapa. Lakini, kama kuna watu ambao wanatakiwa kuangaliwa vilivyo na serikali za ugatuzi, ni MCAs . Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha na aibu kuona kwamba jopo la Ms. Mengich ambalo linahusika na mishahara linazembea. Hatujui ni kwa sababu gani. Lakini, ni jambo la kusikitisha leo kuona wale wanaopanga mambo ya mishahara kuweza kumpatia MCA Kshs80,000 kila mwezi ama ikifika mwisho ni Kshs120,000. Wale ambao wameandikwa ndani ya kaunti kama Mawaziri ambao hawakuchaguliwa na wananchi, hawajui hata kutafuta kura moja, wanapendelewa na kupewa maofisi, na magavana. Wamepewa magari, walinzi, makatibu na wanapikiwa chai saa nne, ilhali, MCAs ambao walitafuta kura kutoka kwa wananchi hawapewi. Ukiangalia tofauti zao ni kwamba yule aliyepewa kazi, chai na gari anaambiwa kazi yake itakuwa kuzunguka ama kuangalia maswala kulingana na wizara yake. County ExecutiveCommittee Member (CECM) anapata Kshs400,000. Hii ni mara nne ama tano zaidi ya MCA. Hii ni makosa na dhambi. Ni muhimu Ms. Mengich aje hapa tuwe na date na yeye. Ninataka kumwambia kwa kinaga ubaga ya kwamba aliyofanya ni dhambi kwa MCAs. Ikizidi sana, inatakikana CECM wapate Kshs80,000 na MCAs wapate Kshs400,000."
}