GET /api/v0.1/hansard/entries/1244901/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1244901,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1244901/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Marupurupu wanayopata ni machache sana kulingana na hali ya maisha ilivyo hususan kwa wale ambao wako katika miji mikubwa na miji midogo pia. Tukiangalia, kwa mfano, katika Kaunti ya Mombasa, Wabunge hawa wa Bunge la Kaunti ya Mombasa wanahitajika kupata ofisi na nyumba ambazo zinastahili hadhi yao. Nyumba hizi haziwezi kukodishwa bila pesa. Kwa hivyo, yale marupurupu wanayopata hayawawezeshi kukabiliana na maisha kisawasawa. Ndio mara nyingi, wanapatikana wakihujumu kazi zao kupitia kwa ile ruzuku ndogo ndogo wanazopata kutoka kwa wakuu wa kaunti."
}