GET /api/v0.1/hansard/entries/1245351/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1245351,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1245351/?format=api",
    "text_counter": 65,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu ya 53(1), kuomba kauli kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Leba na Ustawi wa Jamii kuhusu Maslahi na Ustawi wa Mabaharia Nchini Kenya. Katika Taarifa hiyo, Kamati iangazie yafuatayo:- (1) Ieleze ni hatua gani Serikali inachukua kuhakikisha uzinduzi rasmi na utendakazi wa Baraza la Mishahara ya Wafanyakazi wa Baharini, ikizingatia kwamba mabaharia wanasalia kuwa wenye kipato duni nchini Kenya. (2) Iarifu Seneti sababu zinazosababisha ucheleweshaji wa uchapishaji wa vitambulisho vya mabaharia, ikieleza kwa kina ni mipango gani Serikali inafanya kuhakikisha zoezi hilo linatekelezwa kwa upesi ili kuwapa fursa mabaharia kuweza kuingia nchi mbalimbali ulimwenguni. (3) Ipendekeze utekelezaji wa sera ya mgao wa mshahara wa mabaharia na kuwalazimisha wamiliki wa meli kutuma asilimia sitini ya mshahara kwenye akaunti za mabaharia hao nchini Kenya zikiwa katika sarafu ya dola. (4) Kupendekeza kuajiriwa kwa wakaguzi wa wafanyakazi wa baharini mahsusi wakusaidia kufuatilia maslahi ya mabaharia wanapotoka safari. Asante, Bw. Spika."
}