GET /api/v0.1/hansard/entries/1245399/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1245399,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1245399/?format=api",
    "text_counter": 113,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada wa Ugavi wa Raslimali kwa Kaunti zetu. Mgao wa Raslimali za Kaunti 2023 ni sheria muhimu ambayo inagawanya fedha zinazotoka kwa Serikali Kuu kwenda kwa serikali gatuzi. Bunge hili lilipitisha Mswada wa Division of Revenue Act (DORA) ambayo ilileta Kshs385.425 billioni, kutoka kwa Serikali Kuu Kwenda kwa serikali za kaunti. Ijapokuwa sheria hii ilipita shingo upande, ndio sheria ambayo iko. Kwa hivyo, sheria ambayo tunaijadili kwa sasa, imeundwa ikizingatia kwamba pesa zitakozota kutoka Serikali kuu kuja kwa serikali za kaunti ni Kshs385.425 billion. Ugavi wa rasilimali hii umezingatia mfumo wa tatu wa kugawanya rasilimali, ambao ulipitishwa na Bunge hili Septemba, 2020. Katika vipengele ambavyo vimejadiliwa, mgao wa msingi, yaani basic share, unachukua asilimia 20; wingi wa watu,"
}