GET /api/v0.1/hansard/entries/1245401/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1245401,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1245401/?format=api",
    "text_counter": 115,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "asilimia 10; ukubwa wa ardhi, asilimia nane; ukulima, asilimia 10; afya, asilimia 17, barabara, asilimia nane; ukuaji wa miji, asilimia tano; na umaskini, asilimia 14. Katika kujadili wa Mswada huu, Kamati yetu ilipata fursa na kuchukua maoni kutoka kwa Baraza la Magavana, Wizara ya Fedha, Tume ya Ugavi wa Rasilimali na washikadau wengine. Vile vile, Kamati ilipata maombi kutoka kaunti 17 ambazo zilitaka kuongezwa pesa za msingi kutoka mwaka 2023/2024. Baadhi ya mambo yaliyozungumziwa na mabunge ya kaunti ni pamoja na maswala ya usalama katika kaunti zilizo mbali. Kwa mfano, Kaunti ya Mandera inagharamika pakubwa kupeleka usalama wanapofanya public participation wanapojadili miswaada yao. Maswala ya ujenzi wa majengo ya mabunge ya kaunti pia ni gharama. Vilevile, kununua vifaa vya kisasa vya HANSARD ni donda sugu katika kaunti ambazo zimejenga bunge mpya. Ujenzi wa ofisi za Wajumbe wa Mabunge ya Kaunti pia ni gharama nyingine. Ofisi zenyewe zinatakiwa kuwa na samani na kadhalika. Tuliangalia haya mambo hayo kisha tukatoa mapendekezo kwamba fedha wanazogawiwa ziongezwe, wananchi wahudumiwe vizuri. Tumeona pia Tume ya Ugavi wa Rasilimali imetoa mwongozo kuhusu idadi ya wafanyikazi wanaopaswa kuandika kazi na mabunge ya Kaunti. Bw. Spika, imefika wakati ampapo ipo haja ya kuangalia upya maswala ya wafanyikazi wa kaunti. Kaunti zetu zimenawiri na kamati zimeongezeka. Kamati zile zinasaidia kuhakikisha kwamba fedha zinazotumwa zinatumika vizuri. Ikiwa mabunge ya kaunti yatakuwa na unyonge wa kufanya first oversight, matatizo mengi ambayo yangetatuliwa huko yataletwa katika Bunge hili la Seneti. Itakuwa bora iwapo hayo matatizo yatatatuliwa huko na kuhakikisha kuna haki na usawa katika ugavi wa rasilimali hiyo. Mabunge ya kaunti yanazidi kukandamizwa na Serikali za Kaunti, kwa sababu fedha zinapitia kwa County Treasury ndio zifike kwa Wajumbe wa Mabunge ya Kaunti. Hili swala linafaa kuangaliwa upya katika sheria ya Public Finance Management (PFM) Act, ndiposa bunge la kaunti liwe na fedha zake tofauti na County Executive. Tukifanya hivi, kazi za kaunti hazitalemaa kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Mswada huu ni muhimu katika uendeshaji wa kaunti zetu. Kama alivyosema Mwenyekiti wa Kamati yetu; ni lazima tuupitishee kabla ya mwisho wa mwezi huu ili mabunge ya kaunti yatakapojadili bajeti zao, yazingatie pesa kutoka Serikalii Kuu. Hivyo, watajumuisha fedha watakazokusanya katika maeneo yao, ili kuhakisha huduma hazilemei. Ripoti zilizoko ni kuwa zaidi ya kaunti 14 zimefunga kazi kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Ni muhimu Serikali izingatie mpangilio wa ugavi wa pesa unaopitishwa na Bunge hili, wakati wanapotuma pesa katika kaunti zetu. La sivyo, huduma za kaunti zitalemazwa halafu ndoto ya ugatuzi na huduma kwa kila mwananchi itafifia. Kwa hayo mengi, ninaunga mkono Mswada huu."
}