GET /api/v0.1/hansard/entries/1245508/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1245508,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1245508/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Katiba mpya ilipopita, kulibuniwa Consolidated Fund ama hazina ya kitaifa. Tume ambayo inahusika katika kugawanya hizi pesa mara mbili kwa serikali ya Kitaifa na serikali za kaunti ni CRA. Tume hii ikipitisha mfumo wa ugavi wa pesa kwa serikali ya Kitaifa na kaunti kwa sheria inayoitwa Division of Revenue Act (DORA), Wakenya walisema kwamba ni vizuri kuwa na wawakilishi ama wabunge wa Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti ili kupiga msasa sheria ile. Wiki kadhaa zimepita tangu kupitisha DORB. Baada ya kugawanya pesa mara mbili, pesa za kwenda kwa magatuzi inagawanywa mara 47, kwa sababu magatuzi ni 47."
}