GET /api/v0.1/hansard/entries/1245512/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1245512,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1245512/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "kwa sababu ya ule mfumo uliopendekezwa. Kaunti zingine zilikuwa zinapoteza pesa. Tuling’ang’ana na kukubaliana kwamba tutumie formula ama mfumo wa pili wa kugawanya pesa. Hii leo katika hii sheria DORB, Ksh385.4 bilioni imependekezwa kuenda kwa magatuzi. Kati ya hizi pesa, asilimia 14.5 ama Ksh35.9 billion zimeenda kwa countyassemblies. Bi. Spika wa muda, bila kuongea sana kuhusu undani wa CARB, ningependa kusema kwamba magatuzi ni mfumo wa serikali ambao ni mpya. Mfumo huu umekuwa kwa muda wa miaka 13 lakini umekumbwa na changamoto si haba. Nafikiri katika kuongea kwangu na kuchangia huu Mswada, ni vyema niangalie zile changamoto ambazo zimekumba serikali zetu za ugatuzi."
}