GET /api/v0.1/hansard/entries/1245513/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1245513,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1245513/?format=api",
"text_counter": 227,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Changamoto ni nyingi na ya kwanza ambayo inafanya ugatuzi usinawiri ni kucheleweshwa kwa kutolewa kwa mgao kwa magatuzi. Hivi sasa, serikali za magatuzi zinadai pesa nyingi za mwaka wa kifedha 2022/2023 ambao unaisha mwezi huu. Hata hizi pesa zikiachiliwa na Hazina ya Kitaifa, bado hakutakuwa na muda wa magavana kuzitumia. Kucheleweshwa kwa mgao kwa magatuzi kunapelekea kuwa na huduma duni. Kwa mfano, hospitali hazina madawa na vifaa vya kutibu. Wafanyikazi, madaktari na walimu hawajalipwa. Hivyo basi, huduma zitakuwa duni kwa sababu wafanyikazi hawana motisha. Kama daktari huwezi kufanya kazi ukiwa na motisha ikiwa haujalipwa mshahara. Motisha umekuwa chini kwa wengi. Hata kama wangekuwa na motisha na hakuna dawa na vifaa vya kufanya kazi kule hospitalini, huduma zingekuwa ni duni kabisa. Vilevile, kuna changamoto nyingine tumeiona, na Kiongozi wa Wengi Sen. Cheruiyot aliiangazia vizuri sana. Alisema kwamba tumepeleka pesa kwa kaunti lakini shida imekuwa ni kuajiri watu wengi kupita kile kiwango ambacho kimewekwa na"
}