GET /api/v0.1/hansard/entries/1245515/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1245515,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1245515/?format=api",
    "text_counter": 229,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "sheria. Sheria imesema asilimia 35 ya zile pesa zinazoenda kwa magatuzi itumike kwa uajiri lakini kaunti nyingi zimeajiri watu kupita kiasi. Wengine wametumia asilimia 40 na 50. Kwa mfano, Kaunti yangu ya Taita Taveta, tuko kwa asilimia 52 ya ule mgao unaenda kwa kaunti yetu. Kama tunahitaji kufanya maendeleo na kile kiwango kilichowekwa ni asilimia 35, tukilipa zaidi, zile pesa zinazobaki za operation s inakuwa kama asilimia 10 peke yake. Ni vizuri kama Seneti tuhimize kaunti zetu na tuwalazimishe kufuata sheria za kuajiri. La sivyo, pesa zote zinazoenda kwa kaunti zitatumika kuajiri na maendeleo yatakuwa duni. La tatu ni ufisadi ambao umekuwa donda ndugu katika kaunti zetu. Dhamana ya pesa zinazoenda katika kaunti nyingi hazionekani. Ile miradi inayofanywa na kaunti, bei yake iko juu sana kupita kiasi. Nilijaribu kulinganisha zile pesa, kwa mfano, za kujenga darasa kwa mgao wa National Government - Constituencies Development Fund (NG-CDF) na za kaunti. Unapata darasa inajengwa na Ks1.2 milioni katika NG-CDF, lakini madarasa mengi yanayojengwa na serikali za kaunti ina gharama ya Ksh2.5 milioni. Unashangaa wakandarasi ni wale wale. Kwa nini serikali za kaunti zinatumia pesa nyingi zaidi katika kandarasi hizo? Ni kwa sababu, katika kufanya bajeti ya miradi, wameweka pia pesa ya ufisadi. Donda ndugu lingine lililoko katika kaunti katika uajiri ni kwamba kuna wafanyikazi wengi gushi wanalipwa. Ni vizuri kama Seneti ambayo inafanya secondaryoversight, tuangazie na kutafuta mbinu ambazo zitakomesha ufisadi huu. Shida nyingine ni kwamba kuna maeneo mengine ya magatuzi katika kaunti moja yanayobaguliwa kimaendeleo. Kwa mfano, katika kaunti yangu la Taita Taveta utapata kuna maeneo ambayo yalimpa Gavana support ukilinganisha na yale hayakumpigia kura. Maeneo hayo yanatengwa kimaendeleo. Kwa hivyo, ni vizuri kaunti ziangalie kupitisha sheria itakayo hakikisha kila eneo la kaunti linapata maendeleo bila mengine kuwachwa nyuma. Kama Mswada wa Building Bridges Initiative (BBI) ungepita, tulikuwa tumependekeza kuwe na Ward Equalization Fund ama Ward Development Fund ama sheria ya kuhakikisha kwamba kila wadi inapata pesa zinazowiana na zingine kwa sababu ya maendeleo ili kuhakikisha hakuna eneo lolote katika kaunti limewachwa nyuma. Kuna kaunti zingine nchini tayari wamepitsha sheria ya Ward Development Fund ili kuhakikisha kwamba mgao unaoingia kwa kikapu cha kaunti unaingia kwa kila wadi na kila wadi inapata pesa zake za maendeleo pasipo kutengwa. Changamoto nyingine ni malipo duni ya Wawakilishi wa Wadi. Nashukuru ndugu yangu, Seneta wa Nandi, Sen. Cherarkey, kwa kuleta Ombi kwa Bunge la Seneti kuangazia mambo ya malipo na marupurupu ya Wawakilishi Wadi. Ikiwa unafanya kazi na unalipwa 80,000 kwa mwezi na unatakikana kutunga sheria, kufanya utafiti, kusoma kwa kina na kufanya uangalizi, sina uhakika utakuwa na motisha wa kufanya kazi hiyo. Kama Seneti, hili swala la mshahara na marupurupu ya Wawakilishi Wadi ni swala linalofaa tuliangazie kwa undani. Ni jambo la kuhuzunisha kwa sababu wale Mawaziri wa Kaunti wanapata Ksh400,000. Hata kama kungekuwa na tofauti ya mishahara, labda hawa Wawakilishi wa Wadi wangeanzia, kwa mfano, Ksh200,000 kwenda juu. Huwezi kufanya kazi wakati unaliwap Ksh80,000 kwa mwezi ilhali unatarajiwa kuangalia Ksh5 bilioni. Lazima ukifuatiliwa vizuri na Gavana, utawekwa kwa mfuko. Wawakilishi Wadi wengi Kenya wamewekwa kwa mfuko na magavana. Hawawezi kupumua, hawana sauti"
}