GET /api/v0.1/hansard/entries/1245517/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1245517,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1245517/?format=api",
    "text_counter": 231,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "na wizi unaendelea kwa kaunti zetu na Wawakilishi Wadi hawaongei. Kwa hivyo, hilo ni swala lingine ambalo limepelekea ugatuzi kutonawiri. Swala lingine ambalo tumeliongelea katika Bunge hili ni mfufumko wa bei. Seneta wa Siaya aliangazia hili jambo. Alisema zile pesa zinazotumwa kwa magatuzi hazilingani na mfufumko wa bei kulingana na vile gharama ya maisha imepanda. Ukiangalia kwa ile sheria ya Division of Revenue Allocation Bill (DORB) tuliyopata mapendekezo kutoka kwa County Revenue Allocation (CRA), ilisemekana mfufumko wa bei ilikuwa asilimia nane. Ilitakikana pesa za kwenda kwa kaunti ziwe Ks407 bilioni ili kuangazia mfufumko wa bei lakini tumepeleka Ksh385 bilioni. Kwa hivyo, pesa tulizopeleka kule haziwiani na mfufumko wa bei. Kama kuna bajeti imefanywa mwanzoni wa huu mwaka, kwa mfano, wa kujenga darasa wakati bei ya chuma ilikuwa ni Ksh2000, kwa sasa bei ya chuma imefika Ksh2500, na hatuajaanza mfufumuko na pesa tunayopeleka kwa kaunti, basi kutakuwa na miradi michache itakayofanyika. Kwa hivyo, tungekubaliana wakati mwingine tukiangalia sheria ya DORB ama zile pesa zinazoenda kwa kaunti, tusikize wataalamu wa CRA wanavyosema na walivyofanya hesabu kulingana na mfufumko wa bei na kadhalika. Jambo lingine ningependa kuangazia ni kwamba, baada ya kupitisha hii sheria ya County Allocation Revenue Bill (CARB), kule mashinani kwa kaunti na wao wanafanya bajeti zao kulingana na zile pesa ambazo tumepitisha huku ya kila kaunti kuangalia ile pesa ama makusanyo ama own source revenue ya kaunti. Kuna wazimu unaoendelea kwa kaunti zetu. Unapata kwamba, kufanya biashara kwa kaunti imekuwa vigumu sana kwa sababu vibali vya kufanya biashara vimekuwa juu sana. Bi. Spika wa Muda, kijana mdogo ambaye anaanza biashara ya duka, unamlipisha Ksh40,000 kwa mwaka, ili kuongeza own source revenue . Vijana wetu, akina mama na kadhalika, hawawezi kufanya biashara kwa sababu wanagharamika sana kulipia leseni za biashara ambazo zimewekwa na magatuzi. Nilikuwa ninaangalia Mswada wa Fedha wa 2022/2023 katika Kaunti ya Taita Taveta. Nikapata kwamba mama wa soko anapoleta gunia ya sukumawiki, anatozwa ada ya Ksh30. Ukienda msalani, unatozwa ada ya Ksh10. Nikawa ninajiuliza, jamani, simtamaliza hawa akina mama? Hii ada ya Kshs30 ambayo amelipa, ni ya huduma yaani"
}