GET /api/v0.1/hansard/entries/1245519/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1245519,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1245519/?format=api",
"text_counter": 233,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": ". Huduma zenyewe ni pamoja na choo, usalama na hata maji kama anauza maembe ama sukumawiki ili apate kuosha. Wakati unamlipisha Ksh30 na zingine tena za choo, hivyo ni kulipa ushuru mara mbili, yaani double taxation kwa Kiingereza. Huo wazimu wa own source revenue ama pesa ya makusanyo katika county, umepelekea biashara nyingi kufa. Ni vizuri pia niseme ya kwamba katika huu Mswada wa Fedha, Serikali ya Kitaifa itapelekea biashara nyingi kuharibika. Yule mama mboga ambaye anakusanya Ksh500,000 kwa mwaka, na yeye pia ataingia katika tax brackets kulingana na huu Mswada iwapo utapita. Bi. Spika wa Muda, mtu yeyote ambaye anakusanya Ksh1,390 kwa siku ama Ksh500,000 kwa mwaka, atalipa ushuru kulingana na huu Mswada. Hawa ni mama mboga, mtu wa boda boda na wale watu masikini ambao hii Serikali ya Kenya Kwanza ilisema itawalinda. Huu Mswada ukipita, utawafinyilia. Mfumo wa bottom-up utafinya wale watu wa chini iwapo huu Mswada utapita."
}