GET /api/v0.1/hansard/entries/1247171/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1247171,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1247171/?format=api",
"text_counter": 1586,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Naomba kuunga mkono mjadala huu wa leo. Hazina ya Serikali ya Kitaifa ya ustawi wa Maeneo Bunge imesaidia wananchi wetu haswa katika ujenzi wa mashule, barabara za ndani na mambo mengi sana. Pengine leo tunazungumzia NG-CDF tu, lakini ukiwa pale kwenye kiti, Mhe. Naibu Spika, naomba pia tuweze kusukuma mambo ya National Government Affirmative Action Fund (NGAAF). Mgao huu wa NG-CDF umesaidia sehemu nyingi sana. Nimezunguka Kaunti yangu ya Mombasa, na ningependa kusema kuwa pengine wako na upungufu mahali. Hii ni kwa sababu utapata kuwa katika yale mashule ambayo yamejengwa, kuna mengine ambayo hayana perimeter walls . Msaada umetokea mkubwa sana katika NG-CDF, lakini ingekuwa vizuri ikiwa unaweza kuvuka kidogo ili kusaidia zaidi; kwamba ukijenga shule, basi ujenge pia"
}