GET /api/v0.1/hansard/entries/1247173/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1247173,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1247173/?format=api",
"text_counter": 1588,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": ". Kwa mfano, nimekuwa Jomvu Secondary, ambayo ni shule kubwa, na wale watoto wa kike hawana hata fence . Hamna p erimeter wall na ni boarding school . Nilivyokuwa pale, mwalimu mkuu aliniambia kuwa kulikuwa na malalamishi kuwa pesa hazikutosha. Pesa hizo kidogo zilitosha tu kujenga zile dormitories na laboratories, lakini pia wanahitaji zingine. Wamelia sana kuwa wako katika hali hatari ya kuweza kuingiliwa wakati wowote. Naunga mkono mjadala huu na kuomba kuwa Wabunge waongezewe pesa. Kama akina mama wa NGAAF, tunavyowapigia upato wakati wowote NG-CDF inavyotajwa, tunaomba Wabunge waangalie kuwa akina mama wa kaunti arobaini na saba wanapata mgao wao kwa wakati mzuri. Hadi sasa, hatujapata mgao na hali ziko tata kule mashinani. Kuna mambo ambayo tunataka kufanya kama akina mama wa kaunti arobaini na saba, lakini mgao haujakuja licha ya kuwa ni mdogo sana. Naunga mkono mjadala huu. Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika."
}