GET /api/v0.1/hansard/entries/1247206/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1247206,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1247206/?format=api",
"text_counter": 1621,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kutia sauti yangu haswa kwa miradi ya NG-CDF. Ile miradi inayopatikana na inayoonekana katika maeneo yetu sana ni ya NG-CDF. La kusikitisha zaidi ni kwamba hivi sasa, tunakaribia mwaka mwingine na hatujapata hata robo ya pesa. Ni hatari sana kwa sababu hizi ndizo fedha ambazo zilikuwa zinasaidia maskini asiyejiweza. Lakini sasa hana la kufanya kwa sababu ofisi zetu hazina fedha. Hata sisi tumepeana bursaries lakini mpaka sasa, hatujamaliza kupeana za sekondari na vyuo vikuu kwa sababu hakuna fedha."
}