GET /api/v0.1/hansard/entries/1247209/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1247209,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1247209/?format=api",
    "text_counter": 1624,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "ama namna gani? Hii ni hatari kubwa sana ambayo Wakenya wanapitia. Hali ni ngumu. Ukiangalia shule sasa hivi, vyoo vimefurika. Kipindupindu sasa kinaanza kuingia katika shule zetu na huku unaambiwa ni hazina tunangoja. Lazima watueleze shida iko wapi kwa sababu fedha ziko. Kwa nini haziachiliwi na hii ndiyo miradi ambayo inasaidia wananchi? Nitakupatia mifano katika shule za Kisauni. Kuna Shule ya Msingi ya Kashani ambapo watoto wanasoma mpaka mlangoni. Wanakaa chini. Hata dawati hakuna. Watoto wanapata funza. Zile sakafu zimevunjika na huku ukiitisha fedha, unaaambiwa ungoje hazina. Kinachoendelea ni kitu cha kusikitisha sana. Ukiangalia sasa hivi wakati wa mvua, kuta nyingi katika shule ya msingi ya Magogoni zimeanguka. Ukiangalia Shule ya Msingi ya Bedzimba, utaona ukuta umeanguka, lakini hatuna fedha za kuwasaidia wale watu ili waweze kujiendeleza ama kusoma katika mazingara mazuri. Huyu Waziri wa Fedha ahakikishe kwamba amewachilia hizi fedha kabla hatujaanza kujadili Bajeti inayokuja. Tulipitisha mpaka Bajeti ya Ziada lakini hakuna kitu kimewachiliwa. Upande wangu na Kenya nzima tunajua kwamba NG-CDF imefanya makubwa sana. Kuna watu wamesomeshwa kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne. Kuna wengine wameregeshwa katika vyuo vikuu. NG-CDF ndiyo inawasaidia. Leo, tunasikitika kwamba kwa mara ya kwanza tangu taifa hlii lianze hazina hii, hakuna pesa. Hakuna kitu kinaachiliwa. Hakuna miradi inafanyika, mafuriko yameingia mitaani na hatujui tutafanya nini. Tuhakikishe kwamba tumeisukuma Wizara iachilie hizi fedha ili zisaidie watu wetu. Kwa haya mengi Mhe. Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipatia fursa hii."
}