GET /api/v0.1/hansard/entries/1250622/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1250622,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1250622/?format=api",
    "text_counter": 1720,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mheshimiwa Spika wa Muda. Mimi nimefuatilia kwa kina Bajeti hii ambayo imetengezwa na Kamati ya Bajeti. Lakini nina maswali mengi. Ninafikiri kuwa mambo mengi yamegusiwa na Mheshimiwa ambaye amemaliza kuongea. Imekuwa miezi sita tangu Serikali mpya ichukue uongozi na KRA imeweza kukusanya shilingi trillioni 1.5 kwa muda huo. Lakini, bado NHIF inadai shilingi bilioni ishirini. Shule za umma zinadai shilingi bilioni ishirini na nane. Wazee wa mitaa pia hawakulipwa na wanadai shilingi bilioni kumi. Serikali za kaunti, ambazo ni gatuzi, zinadai shilingi bilioni tisini na tisa. Sasa hivi, wamekopa shilingi bilioni mia sita themanini na tisa. Swali langu ni: je, pesa hizi huenda wapi? Kamati ipige bajeti vizuri na tuhakikishe kuwa pesa hizi zikikusanywa, zinasaidia mwananchi wa Kenya. Mhe. Spika wa Muda, kuna mashimo katika ofisi za umma. Hizi pesa huwa hazifikii huduma lengwa. Kila mwaka, huwa tunatengeneza Bajeti na tunaingia katika mifuko ya Wakenya, tunaichimba na kuwanyang’anya pesa zao. Lakini ikifika kwenye matumizi, haijulikani pesa zimetumika vipi."
}