GET /api/v0.1/hansard/entries/1250623/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1250623,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1250623/?format=api",
    "text_counter": 1721,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti amezungumzia mambo ya uhamiaji. Amesema wametoa Bajeti ya kuweza kutengeneza hizi mashine. Niko katika Kaunti ambayo iko na ofisi ya uhamiaji. Wananchi ndani ya Mombasa wanahangaika sana. Ukienda kuchukua pasipoti, unaambiwa mashine imeharibika na imeenda kutengenezwa Pakistan ama India. Ikiwa vitu hivi huwa vinawekwa kwa Bajeti, kwa nini isinunuliwe mashine mara moja ambayo itatoa huduma kwa wananchi wakienda kutafuta pasipoti? Wananchi wengi wanatafuta ajira kule nje na wengine wangependa kwenda kutibiwa. Hata pale ofisi ya uhamiaji wananchi wanalazimika kungojea kwenye foleni ndefu, miezi sita ama tano, kitambo wafikiwe kupigwa picha tu. Hii yote ni kwa sababu wizi umekithiri katika ofisi za umma. Wananchi ndio wanaumia. Itakuwa sisi tunaunda Bajeti kama hii kila mwaka lakini hatuelewi pesa zinatumika vipi. Mwananchi ni punda na amechoka. Hata tukisema hatutaki kuomba, tujiulize kama yale mapeni tulikuwa tunaomba tulitumia sawasawa ama tuliiba. Kisha, tunarudi kuambia mwananchi kuwa hatuwezi kuomba na itabidi aingie katika mfuko wake alipe ushuru. Akishalipa, tena turudi tuibe hizo pesa. Ni wakati wa Serikali kuchukua msimamo. Tukizidi kufinya wananchi... Serikali yoyote inayotoza wananchi wake ushuru wa juu haipati maendeleo. Serikali nyingi ambazo zimeendelea ziliweka ushuru chini na kuzidisha mazao. Wananchi wakapata mapato ya kutosha. Kisha, wakawa na furaha ya kutoa ushuru zaidi kwa Serikali. Nikiangalia Makadirio ya Bajeti hapa, ninaona tunaomba na kukopa zaidi, lakini mwananchi ndiye anakuja kulipa kutoka kwa mfuko wake kila siku. Inasikitisha sana. Ni wakati sasa Jumba hili lianze kuangalia zile kesi ambazo tulikuwa nazo za rushwa. Watu wameiba pesa na zinachunguzwa na zinamalizika. Isitoshe, majopo yanatengenezwa kila siku. Bajeti ilipitishwa na watu wakaiba pesa. Majopo yanatengenezwa kila siku na kisha yanaenda The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}