GET /api/v0.1/hansard/entries/1250624/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1250624,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1250624/?format=api",
    "text_counter": 1722,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "baridi. Hakuna anayeshikwa wala kuchukuliwa hatua na kurejesha pesa. Kila mwaka, Kamati ya Bajeti itakuwa inatoa Bajeti lakini pesa hazijulikani zinaenda vipi. Nataka kuelezea Kamati ya Bajeti na Ugawaji kuwa imejaribu kufanya kazi nzuri. Kina mama wa kaunti 47 tunajivunia hiyo bilioni moja kwa sababu tumeitafuta sana. Pesa zetu ni kidogo sana. Tunawashukuru kwa hilo. Lakini, ningependa kuona katika Bajeti hii pesa ya kupeleka maji Turkana na Kaskazini Mashariki ili tuweze kukabiliana na njaa. Hawa wananchi watalima mashamba na kupata mazao. Wanyama watapata maji ya kunywa na uchumi utaimarika. Kila mwaka, kule Turkana, Kaskazini Mashariki, na sehemu nyingine nchini, watu wengi hufa kutokana na baa la njaa. Nilifikiria na nikatamani sana Bajeti hii iwe na fedha ambazo zitatumika kupeleka maji sehemu zile. Hivyo, tutaweza kuzalisha zaidi. Mbunge mwenzangu amezungumzia mambo ya ukosefu wa ajira. Watu wengi ambao wanahudumu katika ofisi za serikali wamezeeka. Swali yangu ni: ikiwa watoto wetu watakuwa wanasomea masomo ya uhandisi, ufundi, na masomo tofauti, kwa nini tusiwapatie mwanya wa kuingizwa katika kazi hizi ambazo watu wamehudumu kwa miaka mingi? Tunafaa kuhakikisha kuwa wale waliozeeka wanawafunza wageni jinsi ya kufanya kazi. Iwapo watashika kazi vizuri, basi tuwatoe hawa wazee na kuwapa mgao wao warudi nyumbani kujimudu. Tutahakikisha kuwa vijana tuliowasomesha wanapata ajira. Katika sekta nyingi, wazee wengi wamebaki pale kwa muda mrefu hata ikifika wakati wa kustaafu, hakuna mtu wa kuchukua nafasi zao. Katika Bajeti, wanasema kuwa kwa sababu ya ukosefu wa ajira, wanajaribu kutafuta mwanya wa kuingiza hawa vijana. Mwanya utapatikana ikiwa sisi tutawapa vijana nafasi na msukumo katika Bajeti wa kupata masomo zaidi ili wakiingia pale waweze kuhudumia taifa. Watu wameomba sana pesa nje. Miradi nyingi ya Serikali ambayo imesomwa hapa haijakamilika. Kuna mijengo ambayo imejengwa kutumia pesa za Serikali lakini haitumiki. Hizo pesa zingetumika katika miradi mingine ambayo ingeinua uchumi zaidi. Kuna watu ambao wanaomba kujengewa bwawa lakini pesa zinazopeanwa ni kidogo mno. Ajabu ni kwamba katika Bajeti, pesa zilizokusudiwa kupeanwa huwa ni nyingi. Miradi kama hiyo huwa haikamiliki. Kwa hivyo, kwa upande wangu, Kamati ya Bajeti inapaswa kuweka mradi mmoja na kuhakikisha unakamilika na kufanya kazi kabla ya kufanya bajeti ya mradi mwingine. Na tuhakikishe pia kuwa mradi huo wa pili unakamilika. Tukifuata utaratibu huo, basi hatutakuwa na ubadhirifu. Haitakuwa sawa kuingia mfuko wa Mkenya kila wakati kwa sababu inafaa naye ainuke. Tunamuomba pesa na tunachimba zaidi, halafu tunakuja kutumia fedha hizo vibaya. Kwa kufanya hivyo, hatutakua na uaminifu kwa wananchi wa Kenya. Ninaona bango hili linasoma: ‘‘ For the welfare of society and the just Government of the people’’. Bunge hili linatakiwa kusimamia Mkenya. Tunafaa kumhurumia Mkenya kwa kuweka Bajeti ambayo itakuwa nafuu kwake na siyo ya kumwumiza. Kwa sababu nimeona kidude kimebonyezwa, ningependa kumalizia hapo kwa kusema kuwa Bajeti ni nzuri lakini inahitaji marekebisho ndiyo wasiingie kwenye mifuko ya Wakenya. Asante sana."
}