GET /api/v0.1/hansard/entries/1251151/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1251151,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1251151/?format=api",
    "text_counter": 471,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi. Spika wa Muda, kama naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi tuko na Mswada wa Sen. Tabitha Mutinda. Mambo ya kilimo nchini Kenya yanafaa kuangaliwa na kuzingatiwa kwa makini sana. Hii ni kwa sababu unapofanya kazi yoyote ni lazima ule na unywe. Mambo ya kilimo yametajwa hata katika Bibilia. Naunga mkono Serikali iwe ikiwapa wakulima mbolea kwa bei ya chini. Tunajua wakulima wengi hawana pesa ya kununua mbegu. Kwa hivyo, wawe wakipewa mbegu hizo. Serikali ya Kitaifa inafaa isaidiane na serikali za kaunti. Watu lazima walime katika kaunti zote 47. Kwa hivyo, ni vizuri Serikali za kaunti kushauriana na Serikali ya Kitaifa. Inafaa waalimu wa kufunza watu mambo ya kilimo wawe wanafunzwa vizuri kutoka mashinai, wadi hadi kaunti. Ikiendelea hivyo, Serikali itapata faida kubwa sana. Wakati wa kuvuna, Serikali inafaa itafute soko nchini Kenya ama nchi za ng’ambo. Serikali inafaa ihakikishe kwamba mbegu zisiwe ni zile ambazo zinakaa miezi mingi kabla hazijakua. Tunataka wakulima wapate faida ya mazao yao. Nakumbuka zamani tulikuwa tunazuiea mmomonyoko wa udongo. Wakati ule, marehemu Mhe. Mulu Mutisya ndiye alikuwa mwenyekiti wa tume ya kushughulikia za kuzuiea mmomonyoko wa udogo nchini. Kwa hivyo, tukiwa wadogo, tulikuwa tunaona watu wakija na kupewa chakula ili waweze kuchimba mitaro. Serikali inafaa iangazie mambo ya maji ya visima na mabwawa ya kulima katika kaunti zetu ili tuweze kupata chakula katika kila kona. Ikiwa hata mtu hafanyi kazi, atakuwa anapata faida. Vijana wetu wamekosa kazi siku hizi. Hata hivyo, kila mmoja hata kama amepata shahada ya aina gani, wamekubali kufanya kazi. Serikali inafaa ipatie kaunti pesa nyingi ili ziweze kuajiri walimu wa kilimo wengi ili tuweze kuwa na kilimo bora hapa nchini. Asante, Bi. Spika wa Muda. Naunga mkono."
}