GET /api/v0.1/hansard/entries/1251627/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1251627,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1251627/?format=api",
    "text_counter": 78,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Swala la marupurupu ya mahakimu ni swala nzito sana. Hii ni kwa sababu ndio watu ambao wameidhinishwa na Katiba kujaribu kutatua mizozo katika nchi yetu. Kwa hivyo, ikiwa hawatalipwa malipo ya kisawasawa pamoja na marupurupu ambayo wanatakikana kupata, basi hali yetu ya kupata haki itatatizika. Bw. Spika, mahakimu wengi wanafanya kazi nzuri katika nchi yetu. Vile, kuna mahakimu ambao ni watepetevu na hawatakelezi majukumu yao kisawasawa. Ijapokuwa kuna mfumo mpya wa wao kupeleka hesabu zao kila mwezi, tumeona kwamba imekuwa ni donda sugu katika sehemu ambazo ziko nje ya Mji wa Nairobi na miji mingine mikubwa. Bw. Spika, tumeona ijapokuwa mahakama ilikwenda kwa Serikali wakati Kenya Kwanza ilipochukuwa mamlaka, wameweza kupelekwa pia katika mizunguku ambayo haieleweki. Wanalilia wananchi kila mwezi kwamba hawalipwi marupurupu yao kwa wakati unaofaa. Hatuwezi kudharau kilio cha mahakama kwa sasa kwa sababu inafanya kazi kubwa kabisa ya kuamua kesi za watu binafsi na kesi za Serikali. Kwa hivyo, kulipwa kwa marupurupu haya kwa wakati ni jambo moja nzuri sana. Bw. Spika, tunaona pia huduma ya mahakama ikidorora katika sehemu zingine. Kwa mfano, tukizungumzia Mombasa, kumejengwa jengo jipya ambalo linaitwa Justice Towers. Lakini, jengo lenyewe limejengwa kwa hali ambayo si ya kuridhisha. Wiki iliyopita, tuliona baadhi ya dari zikiangua na kahatarisha maisha ya mahakimu na maafisa wengine ambao wanafanya kazi mahakamani. Bw. Spika, tungependa Serikali iweze kuangalia kwa makini maswala ya mahakimu na mahakama zetu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kisasa na ya kistaarabu ya kuweza kutatua matatizo baina ya wananchi na Serikali au wananchi kwa wananchi. Asante kwa kunipa fursa hii."
}