GET /api/v0.1/hansard/entries/1251893/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1251893,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1251893/?format=api",
"text_counter": 344,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii niweze kukaribisha shule ya upili ya ACK St. James Mayori. Wanafunzi wa ACK St. James Mayori, hii ni Bunge la Seneti. Kazi yetu ni kutengeneza sheria za kaunti na tunajifunza mambo mengi sana. Karibuni ili muone jinsi mambo yanavyoendelea katika Bunge hili. Kama mtasikiza mambo ya walimu na kanisa, mambo ya kujiepusha na pombe, dawa za kulevya na bhangi, mtakuwa Maseneta, Spika na mutaongoza nchi yetu ya Kenya. Namuomba muangalia yale tunayoyatenda hapa kwa sababu nyinyi ndio viongozi wa kesho. Shule ya ACK St. James Mayori iko katika Embu Kaunti. Embu Kaunti tuko na kaunti ndogo nne. Moja ni ya Mbeere South mahali ambapo hakuna maji na barabara. Hii shule ni moja ya zile zinazofanya vizuri sana katika kaunti yetu. Nimekuwa nikiongea mambo ya Embu Kaunti ili tuweze kusaidiwa. Hata wakati kulikuwa na zile pesa za Equalisation Fund, tulikosa. Shule kama hii ingesaidiwa, ingefanya kazi nzuri. Kwa hivyo, naomba ule wakati mwingine, Bunge la Seneti liweze kuangalia mambo ya Embu Kaunti kama vile barabara, maji na kilimo. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}