GET /api/v0.1/hansard/entries/1251948/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1251948,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1251948/?format=api",
"text_counter": 399,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili kuchangia Mswada huu. Kwanza, nawapongeza dada zangu wawili kwa kuleta Mswada huu hapa ili tuweze kujadili na kutunga sheria. Kwa kweli, kuna sheria nyingi zinazosema kuwa ni haki ya kila mtoto ama mwananchi wa Kenya kupata elimu ingawa imekuwa changamoto kubwa kwa watu wanaoishi na ulemavu. Kwa hivyo, wameleta Mswada huu kwa wakati mwafaka. Sasa kuna shule nyingi za watoto walemavu. Kuna moja ambayo imefungwa na zingine ziko katika hatari ya kufungwa. Mimi ni mzazi wa mtoto mlemavu. Tulikuwa tunapata misaada mingi. Leo hii mimi ni Seneta. Kabla niteuliwe kuwa Seneta, nilikuwa nauza viazi. Kuwa na mtoto mlemavu ilikuwa na changamoto kubwa sana. Licha ya kuwa maisha yalikuwa magumu, ilikuwa lazima pia tumtafutie huduma ambazo alihitajika kupata kama hearing aid ambayo ni ghali. Ilikuwa inauzwa Kshs150,000. Ni changamoto nyingi ambazo watoto wanaoishi na ulemavu wanapitia pamoja na wazazi wao. Ni jambo la kutia moyo kuona kwamba kuna watu ambao wamefikiria na kuleta Mswada huu ili uweze kusaidia palipo na pengo. Unanuia kuweka sheria zote kwenye Mswada moja ili haki zao ziweze kuafikiwa. Nampongeza Sen. Crystal Asige kwa kutambua kwamba sio watoto wanaokwenda shule pekee yao wanaohitaji huduma hizi, bali pia watu wazima ambao katika serikali za nyuma hawakuweza kupata fursa ya kupata masomo na huduma ambazo zinazungumziwa hapa. Mswada ulipokuwa ukisomwa, niliskia ikisemwa kuwa kutakuwa na marekebisho kuhusu technical and vocational trainings ambazo zinaendelea katika taifa letu ili wao pia waweze kufaidika kwa sababu hata wao ni Wakenya. Yale ambayo Sen. Mumma amesema ni kweli. Alisema kuwa sisi wazazi wa watoto walemavu tumekuwa tukipokea usaidizi kutoka kwa wafadhili na wala si Serikali. Ningependa kumtambua na kumpongeza bwana mmoja kutoka kule Mombasa. Anaitwa Hasubhai wa Mombasa Portland Cement. Amekuwa akipeana Kshs7,000 kwa kila familia baada ya kila miezi mitatu. Huyo mfadhili wetu amekuwa pia akilipia wanafunzi karo ya shule na kutoa huduma nyingine ndogo ndogo kwa watoto walemavu. Serikali ya Kenya Kwanza inafaa kukumbatia Mswada huu. Isichukuliwe kuwa watu wanaoishi na ulemavu wanapenda kuombaomba ama kutarajia wafadhili na wala si Serikali kuwafanikishia au kuwapa huduma ambazo zinastahiki kupewa na Serikali."
}