GET /api/v0.1/hansard/entries/1252372/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1252372,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1252372/?format=api",
"text_counter": 368,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa hii fursa ya kuchangia Mjadala huu wa kumwondoa mamlakani naibu wa Gavana wa Kaunti ya Siaya. Ninakubaliana na Senate Business Committee (SBC), kuwa tuende njia ya Kamati. Njia hii inahusisha watu wachache na wanapata fursa ya kuangalia yale mashtaka kwa undani. Nilikuwa na fursa ya kumwondoa maamlakani Gavana wa Kaunti ya Meru na ninakubaliana mia kwa mia, kwamba hii ndio njia mzuri zaidi. Nilitarajia kuwa kati ya wale Maseneta waliowekwa katika Kamati hii, kungekuwa na mmoja ambaye angalau alikuwa katika ile Kamati nyingine kwa sababu ya kumbukumbu ya taasisi. Kwa sababu hamna yeyote, basi maafisa, hasa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria katika Bunge la Seneti, amekuwa na umuhimu sana katika kuangazia kumbukumbu za taasisi katika Kamati hizo. Kuna sheria inayoangazia kuondolewa mamlakani kwa magavana, manaibu wao na pia maspika. Sijui huo Mswada umefika wapi lakini ni vizuri uletwe hapa, ili uangazie njia mwafaka ya kuwaondoa mamlakani maafisa wa serikali na kadhalika. Niko na uhakika ya kwamba kamati hii italeta ripoti nzuri na watu wa Kaunti ya Siaya watapata haki yao kwa sababu wanahitaji huduma wala sio malumbano. Fahali wawili wanapopigana, basi nyasi ndizo huumia. Muda wa kuwaondoa mamlakani magavana umekuwa mfupi sana. Wanaoumia ni wanakamati. Hata hivyo, ningependa kuwatia moyo wafanye hivyo. Mswada wa"
}