GET /api/v0.1/hansard/entries/1252415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1252415,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1252415/?format=api",
    "text_counter": 411,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kuanzia mwanzo, naunga mkono Hoja hii kwa kuteuliwa kwa Kamati Maalumu ya kuangazia maswala kumwondoa ofisini Naibu wa Gavana. Bw. Spika, ni wazi dhahiri shahiri ya kwamba Kamati ya watu wachache itakuwa na muda mzuri ya kuangalia hayo maswala kwa kindani kuhusu mashtaka ambayo yameletwa dhidi ya Naibu Gavana wa Siaya. Bw. Spika, nina imani na Maseneta wote ambao wameteuliwa kuangalia hayo maswala. Kile ambacho ningependa kuwaambia ni kuwa wasiingize maswala ya siasa, waangalie mashtaka ambayo yameletwa na gatuzi hilo; wayaangalie kwa undani na walete ripoti ambayo hata sisi hatutakuwa na budi kuiunga mkono. Hii ni kwa sababu, Seneti ni Bunge ambalo limepewa majukumu ya kisheria ya kushughulikia maswala hayo. Watu wa Siaya, tegemeo lao ni Seneti hii. Wana imani kwamba Maseneta waliochaguliwa, wakiwemo; Sen. Tabitha Mutinda, Sen. Omogeni na wote ambao wamechaguliwa--- Nina uhakika nikiangazia kwanza, kama vile Sen. Gataya Mo Fire, alifanya kazi katika gatuzi la Tharaka-Nithi, ana uzoefu na ujuzi wa kuweza kuangalia masuala hayo kwa undani kwa sababu yeye amefanya kazi katika gatuzi moja. Kwa sababu gatuzi zote zilizoko katika Jamhuri ya Kenya zinafanya kazi visawa, ninajua wataongazia vizuri na wataweza kuangalia maswala haya vizuri. Pengine tu kwa maoni yangu, Seneta ambaye ni Kiranja wa Wengi Bungeni, wakati alipokuwa akiangazia maswala ya gavana aliyekuwa ameletwa, Wakenya wengi walisema ya kwamba alionekana amebobea katika maswala ya kisheria kuliko masuala ya udaktari. Pengine angetembea pale ndio aweze kuongeza ule ujuzi pale ndio tuweze kupata matokea ambayo ni mazuri zaidi; matokea ambayo yatakapoletwa hapa, hata watu wa Siaya watakuwa wanafurahia ya kwamba Seneti imefanya vile ambavyo wangetaka mambo yao yafanywe. Vile ambavyo uamuzi utakavyofanywa, kusiwe na mtu yoyote atakayesema kwamba siasa zilifanywa au Naibu Gavana amengandamizwa ama vile. Hata yeye mwenyewe atakubali matokeo hayo. Bw. Spika, naunga na nashukuru. Asante."
}